Ripoti ya mwaka 2023

Kuleta Matumaini kwa Mioyo Midogo: Uchunguzi wa Moyo kwa Watoto na Mission za Operesheni Tanzania (Januari hadi Desemba 2023).
Utangulizi:
Mwaka 2023, The One New Heart Tanzania iliendelea na dhamira yake ya kuleta matumaini na uponyaji kwa watoto wenye matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo. Mwaka huo ulikuwa na mission zenye matokeo makubwa, ushirikiano wa kimkakati, hatua muhimu za kifedha na maono ya ukuaji endelevu.
Mafanikio na hatua muhimu za mission:
Mission ya kuwafikia watoto kwa uchunguzi wa moyo (Machi 2023):
- Tulishirikiana na For Hearts and Souls kutoka Marekani, na tukawafikia watoto 249 waliohitaji huduma za moyo.
- Tuliwachunguza watoto 171 katika St. Francis Referral Hospital Ifakara na watoto 78 katika Benjamin Mkapa Hospital Dodoma.
- Tuliwabaini watoto 30 wanaofaa kufanyiwa operesheni za moyo za kufungua kifua na catheter ya moyo.
- Tulijitolea kutoa huduma shufaa kwa watoto wenye matatizo magumu ya moyo ya kuzaliwa nayo.
Mission ya operesheni na catheter (Novemba 2023):
- Tulifanikiwa kufanya operesheni nane (8) za moyo kwa watoto katika Benjamin Mkapa Hospital Dodoma.
- Tuliwachunguza watoto 248, na kufikisha jumla ya watoto 901 tangu mission ya kwanza ya Machi 2021.
- Tuliwafundisha zaidi ya wafanyakazi 20 wa hapa nchini, na kuongeza uwezo wa ndani wa kuhudumia wagonjwa siku zijazo.
- Tulishirikiana vizuri na mashirika ya ndani yasiyo ya faida: Maternal Care Foundation, Tanzania Epilepsy Organization na Music for Hope Tanzania.
Ushirikiano wa kimkakati:
- Tulifanikiwa kuhuisha usajili wa shirika ili kuongeza wakurugenzi watarajiwa.
- Tulisajili One Heart Safaris Limited kwa ajili ya kutafuta fedha za shughuli za kuokoa maisha na uendeshaji wa shughuli za ndani, kuanzia Januari 2024.
- Tulianzisha ushirikiano na Maternal Care Foundation (McF), shirika la ndani lenye malengo yanayofanana na yetu.
- Tulialikwa na Ofisi ya Rais Zanzibar kuanzisha huduma ya uchunguzi wa moyo kwa watoto katika hospitali za KMKM na JKU. Dkt. Beatus atafanya uchunguzi wa moyo bure kila wiki kwa watoto wa Zanzibar mara hospitali itakapoandaa chumba cha uchunguzi.
Taarifa za fedha:
- Tulifanikiwa kuandaa taarifa za fedha na za kodi kwa miaka 2019 hadi 2021.
- Ukaguzi wa hesabu za mwaka 2022-2023 unaendelea, na taarifa zitatolewa kufikia Mei 2024.
Michango na ushirikiano:
- Jumla ya michango mwaka 2023: TZS 33,102,016.35
- Jumla ya kodi mwaka 2023: TZS 843,580.98
- Michango halisi mwaka 2023: TZS 32,258,435.37
Orodha ya wafadhili:
- Calvary Chapel South Maui - USA
- Shirika la For Hearts and Souls - USA
- Container Concepts Limited - Tanzania
- Ark Associates Limited - Tanzania
- Theresia Sembua - Tanzania
- Esther Juliana Lukwago - Uganda
Kubaini hatari na mikakati ya kuzipunguza:
Hatari kuu:
- Michango midogo kutoka ndani ya nchi.
- Maandalizi na mawasiliano yasiyoridhisha wakati wa mission.
- Kutegemea michango kutoka nje ya nchi.
Mikakati ya kupunguza hatari:
- Kuimarisha ubia na ushirikiano wa ndani.
- Kuiongezea nguvu timu ya ndani kwa kuwaleta wanachama wapya wenye uwezo, ujuzi, maarifa na utaalamu.
- Kuboresha mawasiliano na ufuatiliaji.
- Kuongeza vyanzo mbalimbali vya fedha.
Mipango ya dharura:
- Kuandaa mikakati mbadala ya kutafuta fedha.
Mwelekeo wa kifedha kwa mwaka 2024:
- Makadirio ya mapato kwa mwaka 2024 yanalenga kukamilisha ujenzi wa nyumba ya watoto ya ghorofa 2 huko Dodoma, ambayo msingi wake tayari umeshawekwa.
- Kuanzisha kliniki ya moyo inayotembea kwa ajili ya watoto.
Mgawanyo wa bajeti kwa mwaka 2024:
- Bajeti ya mwaka 2024 inajumuisha fedha za kukamilisha ujenzi wa nyumba ya watoto ya ghorofa 2 huko Dodoma na,
- Kununua gari, mashine ya echo inayobebeka, kitanda cha kuchunguzia wagonjwa, kifaa cha kufuatilia hali ya mgonjwa (patient monitor), mashine ya ECG na printa kwa ajili ya kliniki inayotembea.
Hitimisho:
Tunatoa shukrani zetu za dhati kwa wafadhili wetu kwa msaada wao usiokoma na ukarimu wao, ambao umetuwezesha kuendelea kuleta matumaini na uponyaji kwa watoto wenye matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo.
The One New Heart Tanzania inaendelea kusimama imara katika dhamira yake ya kuleta mabadiliko katika maisha ya mioyo hii midogo, na tunatarajia kuendelea kupata msaada wenu mwaka 2024.
Habari zaidi
Habari zote
Siku ya Moyo Duniani 2026: zijue dalili za magonjwa ya moyo kwa watoto
Katika Siku ya Moyo Duniani tunaiomba kila familia, kila mhudumu wa afya na kila kiongozi Tanzania kuchukua hatua mapema dhidi ya magonjwa ya moyo kwa watoto. Vipimo vya mapema hubadilisha maisha ya mtoto.
Soma zaidi
Colors to Save Hearts yazinduliwa Tanzania
The One New Heart Tanzania imezindua Colors to Save Hearts, mpango wa miezi 12 unaolenga kupunguza Rheumatic Heart Disease (RHD) miongoni mwa…
Soma zaidi
Moyo kwa kila mtoto: The One New Heart Tanzania yajiunga na Global Heart Hub
Tuna furaha kuwajulisha kwamba tumejiunga rasmi na Global Heart Hub, muungano wa kwanza wa kimataifa wa mashirika ya wagonjwa wa moyo, unaotetea…
Soma zaidi