Mission ya uchunguzi wa moyo kwa watoto katika Mbeya Zonal Referral Hospital - Machi 2024

Utangulizi: Lengo la mission hii ya siku tatu ya uchunguzi wa moyo kwa watoto katika Mbeya Zonal Referral Hospital lilikuwa kuwapima watoto wenye umri wa miaka 0 hadi 14 kutoka mikoa saba ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, yenye watu zaidi ya 10,000,000.
Mission hii ni sehemu ya programu ya miaka mitatu ya kupima moyo kwa watoto nchi nzima, inayolenga kuwafikia watoto wa maeneo yote ya nchi, hasa wale ambao bado hawajapata huduma hii muhimu. Pia inalenga kupima kiwango cha magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo, kuboresha ugunduzi wa mapema na kutoa matibabu ya moyo kwa gharama nafuu kwa watoto hawa.
Asanteni wadau na wafadhili wote kwa msaada wenu uliofanikisha mission hii. Kampuni na taasisi zilizofadhili mission hii ni pamoja na Mbeya Zonal Referral Hospital, Container Concepts Limited, Pacific Diagnostics, Tembosoft Limited, Ark Associates na Maternal Care Foundation.
Muhtasari wa mission: Lengo letu lilikuwa kutoa uchunguzi wa moyo bila malipo kwa watoto kutoka mikoa saba ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini. Malengo mahususi yalikuwa kuongeza uelewa, kujenga uwezo, kupima ukubwa wa tatizo la magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo na kuwapa watoto waliopimwa njia za kupata matibabu.
Maandalizi: Maandalizi ya mission yalihusisha kuchangisha fedha za mission, kisha kushughulikia maombi mbalimbali (kibali cha kuendesha mission katika Mbeya Zonal Referral Hospital, viza kwa daktari wetu kutoka nje ya nchi na leseni ya kufanya kazi). Mipango ya safari ilijumuisha kukata tiketi za ndege na kuandaa chakula na malazi kwa timu. Pia, tulilazimika kutafuta mashine ya echo kutoka taasisi nyingine kwa ajili ya mission, na kwa bahati nzuri tuliipata kutoka Pacific Diagnostics Limited. Tulipanga kuisafirisha mashine hii kutoka Dar es Salaam hadi Mbeya kwa gari binafsi la kukodi, kwa sababu mashine hiyo haikuwa ya kubebeka (ina uzito wa kilo 75), na tungelazimika kufuta baadhi ya tiketi zetu za ndege za ndani ili kuisindikiza mashine hadi Mbeya, safari ya barabarani ambayo ingeweza kuchukua hadi siku mbili. Kwa bahati nzuri, Mbeya Zonal Referral Hospital ilitupa mashine ya echo.
Utekelezaji: Daktari wetu kutoka nje ya nchi aliwasili Dar es Salaam kwa wakati akitokea Bangalore, India, asubuhi ya 9 Machi 2024. Tulifanya kikao kifupi cha bodi katika ofisi yetu ya Dar es Salaam, tukala chakula cha mchana, kisha tukaelekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa safari ya jioni kwenda Mbeya. Tulifika salama Mbeya kupitia Uwanja wa Ndege wa Songwe, na dereva wa hospitali alitupeleka kwenye malazi yaliyokuwa karibu sana na geti la hospitali.
Tulianza uchunguzi tarehe 10 Machi (nusu siku) na tukafanya kikao kifupi cha utambulisho na mkurugenzi wa huduma za matibabu wa hospitali. Siku hiyo tuliwapima watoto 17 tu kwa sababu ilikuwa Jumapili.
Siku iliyofuata tulikutana na Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali na kumweleza mpango wa ushirikiano wa kuanzisha programu endelevu ya matibabu ya moyo hospitalini hapo. Siku hiyo tuliwapima watoto wengi zaidi na ilitubidi kuendelea hadi jioni. Kisha tulipata nafasi ya kutembelea sehemu kubwa ya hospitali na kujionea miundombinu ambayo hospitali imewekeza kwa ajili ya programu ya matibabu ya moyo.
Siku ya 3, tuliendelea na uchunguzi tangu asubuhi, sambamba na wasilisho fupi kutoka kwa timu ya upasuaji kuhusu mpango mkakati wa kuanzisha huduma za operesheni za moyo hospitalini hapo.
Ushiriki na mwitikio: Tulifanikiwa kuwapima watoto zaidi ya 100. Kwa makadirio, katika kila kundi la watoto 10 tuliowapima, watoto kama 4 walionekana kupata echo yao ya kwanza ya moyo kwa wakati unaofaa baada ya kuzaliwa. Watoto kama 6 walichelewa kupata echo yao ya kwanza ya moyo, jambo linaloweza kuonyesha kuchelewa kugundulika au kuchelewa kufanyiwa uchunguzi wa kitabibu. Bado tunahitaji kufanya echo zaidi ili kuthibitisha makadirio haya. Timu yetu ilijumuisha wanachama 2 wa The One New Heart Tanzania, daktari bingwa 1 wa moyo wa watoto anayetibu kwa catheter (interventional pediatric cardiologist) kutoka India, daktari bingwa 1 wa watoto, daktari bingwa 1 wa moyo wa watoto, daktari bingwa 1 wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu, daktari wa magonjwa ya ndani, mhandisi wa vifaa tiba, wauguzi 2, afisa uhusiano na msajili.
Matokeo ya uchunguzi: Jumla ya watoto 104 walipimwa. Tumeahidi kugharamia matibabu ya watoto 5 wanaohitaji operesheni ya haraka. Wengine wenye hali mbaya watapata huduma ya tiba shufaa (palliative care), na wengine zaidi watafanyiwa uchunguzi baada ya miaka 1-3.
Matokeo na hadithi za mafanikio: Baadhi ya wagonjwa waliofika kwenye mission yetu walikuja kwa ajili ya ufuatiliaji. Walikuwa wamefanyiwa operesheni miaka michache iliyopita Dar es Salaam, lakini kwa bahati mbaya hawakuweza kuhudhuria kliniki kwa sababu ya umbali mrefu na gharama za kukaa Dar es Salaam.
Shukrani: Tunatambua mchango wa wafadhili, wadau, wanaojitolea na watumishi wa hospitali katika kufanikisha mission hii.
Hatua zinazofuata: Katika mission hii ya uchunguzi, tuliona idadi kubwa ya watoto wenye matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo kutoka mkoa wa Rukwa. Hata hivyo, takwimu zaidi zinahitajika ili kupima kwa usahihi ukubwa wa tatizo la magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo katika maeneo hayo.
Tumejenga mtandao na watoto, wazazi na madaktari, na tuna programu ya ushirikiano ya kupima watoto mara kwa mara, kuelimisha jamii na kutoa mafunzo katika kata na vijiji vya maeneo hayo, ili dalili za magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo ziweze kugundulika na kuripotiwa mara moja.
Hitimisho: Mission yetu ijayo italenga kuendesha programu ya uchunguzi bila malipo na kuwafundisha mafundi na madaktari wa hospitali kufanya echo za kina na kutafsiri majibu yake.
Tunamshukuru kila mmoja wenu, na tunatarajia kuendelea kushikamana katika huduma hizi za kugundua matatizo ya moyo mapema, ambazo huwezesha matibabu kuanza mapema na hivyo kupunguza vifo na maradhi yanayotokana na matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo hapa Tanzania.
Habari zaidi
Habari zote
Siku ya Moyo Duniani 2026: zijue dalili za magonjwa ya moyo kwa watoto
Katika Siku ya Moyo Duniani tunaiomba kila familia, kila mhudumu wa afya na kila kiongozi Tanzania kuchukua hatua mapema dhidi ya magonjwa ya moyo kwa watoto. Vipimo vya mapema hubadilisha maisha ya mtoto.
Soma zaidi
Colors to Save Hearts yazinduliwa Tanzania
The One New Heart Tanzania imezindua Colors to Save Hearts, mpango wa miezi 12 unaolenga kupunguza Rheumatic Heart Disease (RHD) miongoni mwa…
Soma zaidi
Moyo kwa kila mtoto: The One New Heart Tanzania yajiunga na Global Heart Hub
Tuna furaha kuwajulisha kwamba tumejiunga rasmi na Global Heart Hub, muungano wa kwanza wa kimataifa wa mashirika ya wagonjwa wa moyo, unaotetea…
Soma zaidi